Habari

British Airways imesitisha safari za Dar es Salaam kwakuwa ilikuwa ikipata hasara

british airways (600x411)

Baada ya miongo minne ya kutoa huduma nchini Tanzania, hatimaye shirika la ndege la British Airways limeamua kusitisha safari zake za kuja nchini kwa madai kuwa ilikuwa ikipata hasara.

Maelezo kutoka kwa shirika hilo yalisema, “”Dar es Salaam was not performing well from a commercial perspective so we have taken the decision to suspend the route.”

Kwa mujibu wa maelezo hayo, abiria waliokuwa wamebook kusafiri kabla ya March 31 watarudishiwa fedha zao ama kuhamishiwa kwenye ndege zinazoishia Nairobi, Entebbe ama Lusaka.

Uamuzi huo unadaiwa kuwa utaathiri uchumi wa Tanzania kwa namna nyingi ikiwa pamoja na kupungua kwa watalii kutoka nchini Uingereza na mambo mengine.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents