Uncategorized

Buibui arudi kwa kishindo chini ya uongozi mpya

Baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu, muimbaji aliyewahi kutamba nchini, Buibui amerejea tena akiwa chini ya uongozi mpya wa Tanzania Music Power, TMP.

TMP ambayo ni jumuia mpya ya kiharakati iliyoingia rasmi katika kuokoa kizazi cha muziki wa Bongo fleva Tanzania imeingia makubaliano na msanii huyo ambaye jina lake ni Frank Lewis Katende Kivunike.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari TMP imesema imeingia makubaliano na Buibui baada ya kukiona kipaji chake na juhudi zake katika kufanya kazi ya muziki wa kizazi kipya.

“TANZANIA MUSIC POWER inatambua uwepo wa vyombo vya habari na mchango wao katika tasnia ya muziki,hivyo inawaomba wasanii, wanahabari na wadau wote wa muziki kusaidia katika kuwainua wasanii ambao wamechangia kuuweka muziki wa Tanzania ulipo sasa,” imeandika katika taarifa yake.

“Historia ya Buibui ni ndefu sana toka alipo zaliwa mpaka sasa na muda si mrefu TANZANIA MUSIC POWER itatoa kitabu cha maisha ya BUIBUI kuanzia watu aliowahi kushirikiana nao na mpaka kudondoka katika tasnia ya muziki.

BUIBUI amerudi sasa na T.M.P inatarajia kutambulisha wimbo wake mpya ambao utaanza kurushwa hewani rasmi baada ya kumalizika kwa makubaliano ya mwisho na TMP.

Hivyo basi tunapenda kuchukua nafasi hii kuomba watanzania wote kumpokea BUIBUI,tunatanguliza shukrani za dhati kwa watanzania wote.”

Download Here

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents