Tupo Nawe

Bundesliga kuanza kutimua vumbi kesho, Dortmund kuwavaa Shalke 04 

Ligi kuu ya kandanda ya Ujerumani, Bundesliga, inarejea tena mwishoni mwa juma baada kusitishwa kwa karibu miezi miwili kutokana na janga la virusi vya corona.

Kuanza tena kwa ligi hiyo kunaangaliwa kama jaribio juu ya iwapo kandanda na mashindano mengine ya michezo duniani yanaweza kuanza tena chini ya kiwingu cha janga la COVID-19.

Miongoni mwa michezo ya kufungua dimba itayofanyika kesho ni pamoja na mpambano wa kukata na shoka kati ya mahasimu wa jadi Borussia Dortmund na Shalke 04 mjini Dortmund.

Hata hivyo mechi tisa za duru ya 26 ya Bundesliga zitachezwa bila kuwepo mashabiki uwanjani. Ligi nyingine barani Ulaya ikiwemo ile ya Uingereza, Italia na Uhispania zinatarajiwa kuanza tena baadae mwezi Juni.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW