Technology

Bunge la Ulaya lapitisha sheria ya ‘Online copyright’, YouTube yatajwa kuathiriwa zaidi

Bunge la Ulaya wiki hii limepitisha maboresho ya Sheria ya Hakimiliki ambayo yatasababisha mabadiliko makubwa katika matumizi ya internet, yakinufaisha wabunifu kama wasanii na kampuni za habari, huku yakiumiza wamiliki wa mitandao ya kijamii kama Google, ambayo inamiliki YouTube.

Licha ya kuwepo mjadala mkali, wabunge wa Jumuiya ya Ulaya wanaoendelea na kikao jijini Strasbourg, waliishia kupitisha muswada huo kwa kura 348 huku kura 274 zikipinga na wabunge wengine 36 wakiamua kutoshiriki.

Watunga sheria hao wa Ulaya waligawanyika katika suala la hakimiliki, huku wote wakizongwa na kampeni kali ambazo hazijawahi kushuhudiwa za kupinga au kupigia upatu sheria hiyo, zilizofanywa na kampuni hizo kubwa za teknolojia zikishirikiana na wanaharakati wanaotetea uhuru wa matumizi ya internet dhidi ya kampuni za habari na wazalishaji wa maudhui kama wanamuziki.

Tangu kuanza mwaka 2016, kuboresha sheria ya haki miliki kulionekana kama ni hitaji la haraka kwa kuwa sheria hiyo haikuwahi kufanyiwa marekebisho tangu mwaka 2001, yaani kabla ya kuzaliwa kwa YouTube au Facebook. 

Mageuzi hayo yaliungwa mkono kwa nguvu na kampuni za habari na wasanii, ambao wanataka kupata fedha nzuri zaidi kutoka katika mitandao ambayo inaruhusu watumiaji kusambaza kazi zao.

Lakini ilipingwa vikali na kampuni hizo, hasa Google ambayo inatengeneza fedha nyingi kutokana na matangazo yanayowekwa kwenye kazi zinazowekwa kwenye mtandao wake wa YouTube. Pia ilipingwa na wanaharakati wanaotetea matumizi huru ya internet ambao wanahofia kuwa mageuzi ya sheria hiyo yatasababisha kuwekwa kwa vikwazo vingi ambavyo havijapata kutokea.

Kipindi cha kuelekea kura hiyo kilitawaliwa na maandamano, kampuni za habari kuonyesha msimamo kuunga mkono sheria hiyo, huku maelfu ya watu wakiandamana nchini Ujerumani chini ya kaulimbiu ya “Save the Internet (Okoa Internet)”.

Kulikuwa na vitendo vya kuunga mkono mageuzi hayo katika nchi za Austria, Poland na Ureno, wakati magazeti makubwa nchini Poland juzi yalichapisha matoleo yao bila kuweka kitu chochote kwenye kurasa zake za mbele katika jitihada za kusihi wabunge wapitishe sheria hiyo.ayo yanapingwa sana, kampeni zikiongozwa na Julia Reda, mbunge mwenye umri wa miaka 32 kutoka chama cha Pirate. Mbunge huyo anaongoza kampeni ya kupinga vipengele viwili katika sheria hiyo ambavyo ndivyo vinaangaliwa sana.

“Najua kuna hofu kuhusu watumiaji wanaweza kufanya au wasifanye — sasa tuna picha kamili ambayo inahakikisha uhuru wa kuongea, kufundisha na ubunifu wa mitandaoni,” Makamu wa Rais wa Kamisheni ya Ushindani, Andrus Ansip alisema baada ya matokeo.

Naye Reda alisema kura hizo zimekuwa mbaya kwa “uhuru wa internet” na kulaumu wabunge kwa kutofanya marekebisheo kwenye sheria hiyo kabla ya kupiga kura ya mwisho.

Julia Reda, mbunge mwenye umri wa miaka 32 kutoka chama cha Pirate. Mbunge huyo anaongoza kampeni ya kupinga vipengele viwili katika sheria hiyo ambavyo ndivyo vinaangaliwa sana.

Kwanza ni Kifungu cha 13, ambacho kinalenga kuwapa wamiliki wa haki kama kampuni za habari au wasanii, nguvu zaidi katika majadiliano na mitandao kama YouTube, Facebook na Soundcloud, ambazo zinatumia kazi zao.

Chini ya mageuzi hayo, kwa mara ya kwanza sheria ya Ulaya itafanya mitandao hiyo kuwajibika kisheria katika utekelezaji wa haki miliki, ikiwataka kuangalia kila kitu ambacho watumiaji wake wanatuma mitandaoni kuona kama inavunja sheria.

Reda na wafuasi wake wanasisitiza kuwa Kifungu cha Article 13 kitalazimisha mitandao kuweka teknolojia ya kuchuja kazi hizo ambayo itakagharimu fedha nyingi na mara nyingi kusababisha kufuta kimakosa kazi zilizo mitandaoni.

Wanaounga mkono sheria hiyo, wakiongozwa na Axel Voss, wanajibu kuwa teknolojia hiyo ya kuchuja kazi si muhimu lakini hawaelezi ni vipi kampuni zitaweza kufuata kifungu hicho.

Wapinzani wa sheria hiyo wanataka kifungu hicho kiondolewe katika sheria, pendekezo linaloungwa mkono na chama cha walaji barani Ulaya, BEUC.

“Tunaunga mkono kikamilifu malipo sahihi kwa wabunifu, lakini hilo lisiumize watumiaji. Kuna hatari kubwa kwamba sheria mpya itakuwa na madhara zaidi kuliko mazuri.

ayo yanapingwa sana, kampeni zikiongozwa na Julia Reda, mbunge mwenye umri wa miaka 32 kutoka chama cha Pirate. Mbunge huyo anaongoza kampeni ya kupinga vipengele viwili katika sheria hiyo ambavyo ndivyo vinaangaliwa sana.

“Najua kuna hofu kuhusu watumiaji wanaweza kufanya au wasifanye — sasa tuna picha kamili ambayo inahakikisha uhuru wa kuongea, kufundisha na ubunifu wa mitandaoni,” Makamu wa Rais wa Kamisheni ya Ushindani, Andrus Ansip alisema baada ya matokeo.

Naye Reda alisema kura hizo zimekuwa mbaya kwa “uhuru wa internet” na kulaumu wabunge kwa kutofanya marekebisheo kwenye sheria hiyo kabla ya kupiga kura ya mwisho.

Julia Reda, mbunge mwenye umri wa miaka 32 kutoka chama cha Pirate. Mbunge huyo anaongoza kampeni ya kupinga vipengele viwili katika sheria hiyo ambavyo ndivyo vinaangaliwa sana.

Kwanza ni Kifungu cha 13, ambacho kinalenga kuwapa wamiliki wa haki kama kampuni za habari au wasanii, nguvu zaidi katika majadiliano na mitandao kama YouTube, Facebook na Soundcloud, ambazo zinatumia kazi zao.

Chini ya mageuzi hayo, kwa mara ya kwanza sheria ya Ulaya itafanya mitandao hiyo kuwajibika kisheria katika utekelezaji wa haki miliki, ikiwataka kuangalia kila kitu ambacho watumiaji wake wanatuma mitandaoni kuona kama inavunja sheria.

Reda na wafuasi wake wanasisitiza kuwa Kifungu cha Article 13 kitalazimisha mitandao kuweka teknolojia ya kuchuja kazi hizo ambayo itakagharimu fedha nyingi na mara nyingi kusababisha kufuta kimakosa kazi zilizo mitandaoni.

Wanaounga mkono sheria hiyo, wakiongozwa na Axel Voss, wanajibu kuwa teknolojia hiyo ya kuchuja kazi si muhimu lakini hawaelezi ni vipi kampuni zitaweza kufuata kifungu hicho.

Wapinzani wa sheria hiyo wanataka kifungu hicho kiondolewe katika sheria, pendekezo linaloungwa mkono na chama cha walaji barani Ulaya, BEUC.

“Tunaunga mkono kikamilifu malipo sahihi kwa wabunifu, lakini hilo lisiumize watumiaji. Kuna hatari kubwa kwamba sheria mpya itakuwa na madhara zaidi kuliko mazuri.,”

Source: Mwananchi / Theverge

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents