Habari

Bunge laahidi ushirikiano kwa Jaji Mkuu mpya

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amesema kuwa yeye na wabunge watampa ushirikiano Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Hamis Juma aliyeapishwa leo Ikulu jijini Dar es salaam.

Spika Ndugai ameyasema hayo wakati alipokuwa anatoa salamu za Wabunge katika ghafla hiyo ya mukuapisha Jaji huyo, ambayo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Kitaifa.

“Kwa muda wote ulipokuwa Kaimu hukufika hata siku moja bungeni naamini kwamba wewe na timu yako wakati wote mkifika Dodoma karibuni sana Dodoma sisi kama bunge tunawahakikishia ushirikiano mkubwa sana kuhakikisha kwamba kazi za Mahakama kama zilivyo Kikatiba na tunaheshimu sana yale maneno madogo madogo makombora mamoja moja ya bungeni ni vitu vya kawaida waheshimiwa Majaji kule wakati mwingine ndio utamaduni wa huko ,” alisema Spika Ndugai.

Aidha, Ndugai amesema Mahakama inamchango mkubwa kwa wananchi pamoja na taifa kwa ujumla kwa kuwa hicho ndicho chombo pekee kinachoweza kumtetea mnyonge kuweza kupata haki yake kutoka kwa waporaji.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents