Habari

Bunge laweka wazi taarifa za malipo ya fedha za matibabu ya Mhe. Lissu

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Septemba 24, 2017 limetoa ufafanuzi na uthibitisho wa risiti ya malipo ya fedha zilizochangwa na wabunge kwa ajili ya matibabu ya Mhe Lissu ambapo taarifa imeeleza kuwa pesa hizo zilitumwa tarehe 20 Septemba 2017 kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwenda moja kwa moja kwenye akaunti ya Hospitali ya Nairobi.

Bunge limelazimika kutoa taarifa hiyo baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa hospitali ya Nairobi mbaka jana ilisema haijapokea fedha hizo kutoka kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Septemba 22, 2017 Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe alisema kuwa mpaka siku hiyo anatoa taarifa mbalimbali kuhusu Tundu Lissu fedha ambazo wabunge walikuwa wamechanga kwa ajili ya matibabu ya Tundu Lissu zilikuwa bado hazijafika Hospitali Nairobi Kenya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents