Burudani ya Michezo Live

Burna boy azidi kupasua anga, Michelle Obama autaja wimbo wake anaousikiliza akiwa mazoezini

Burna boy azidi kupasua anga, Michelle Obama autaja wimbo wake anaousikiliza akiwa mazoezini

Msanii kutoka nchini Nigeria Damini Ebunoluwa Ogulu alimaarufu Burna boy anazidi kuimarika kimuziki duniani kwani amekuwa miongoni mwa wasanii kutoka barani Afrika ambayo muziki wao unasikilizwa sana duniani.

Ikiwa wiki kadhaa zilizopita rapper kutoka MAREKANI Jay Z aliweka orodha ya nyimbo zake bora anazopenda kuzisikiliza na katika orodha hiyo akiuweka wimbo wa Burna Boy.

Mbali na Jay Z Malkia wa zamani wa taifa la Marekani ambaye alikuwa wa kwanza mwenye asili ya Afrika Michelle Obama, kama mumewe Barack, ameonyesha kupenda muziki wa Burna Boy.

Siku Ya Jumapili, Michelle aliorodhesha nyimbo anazozipenda na miongoni mwa orodha hiyo ameuweka wimbo wa mwimbaji wa Nigeria ‘My Money, My Baby’ kwenye orodha yake akisema huzsikiliza sana na hasa mwaka huu 2020. . Nyimbo hizi huwa zinaonekana kunipa kiboreshaji cha ziada kupitia mazoezi magumu zaidi.

“Aliandika. Aliorodhesha nyimbo nyingi, na Burna Boy alionekana kama namba nne katika orodha hiyo.

Mbali na Michelle Obama kuweka orodha hii ikumbukwe wiki kadhaa zilizopita mume wake na aliyewahi kuwa rais wa Marekani Barack Obama alimuorodhesha Burna Boy pamoja na kijana kutoka lebo ya Mavis record Rema ambapo aliuweka wimbo wa Burna boy Anybody na wimbo wa Rema Iron Man.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW