Habari

Burundi yajitoa rasmi Mahakama ya ICC

Burundi imekuwa ni nchi ya kwanza kujiondoa katika Mahakama ya Kimataifa inayoshughulikia uhalifu wa jinai (ICC).

Hatua za nchi hiyo kujiondoa katika Mahakama hiyo zilianza tangu Oktoba 27 ya mwaka jana kwa kumuandikia barua aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon na hatimaye limeweza kufanikiwa katika kipindi hiki.

Hata hivyo ICC bado ina uwezo kuchunguza uhalifu uliotekelezwa wakati Burundi ilipokuwa mwanachama wa Mahakama hiyo lakini haiwezi kuchunguza uhalifu wowote ambao unaweza kujitokeza siku zijazo.

Nchi nyingine ambazo zilikuwa na mpango wa kujitoa katika Mahakama hiyo ni pamoja na Gambia na Afrika Kusini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents