BurudaniHabari

Bushoke atimkia Bondeni

BushokeMh!? hii nayo kali, msanii Bushoke amekimbilia nchini Afrika Kusini baada ya kuona hakieleweki kuhusu albam yake ambayo ameikamilisha na kuifikisha ubaoni kwa wadosi ambao walishindwa kufikia muafaka katika suala la mkwanja.

BushokeMh!? hii nayo kali, msanii Bushoke amekimbilia nchini Afrika Kusini baada ya kuona hakieleweki kuhusu albam yake ambayo ameikamilisha na kuifikisha ubaoni kwa wadosi ambao walishindwa kufikia muafaka katika suala la mkwanja.

Bushoke ambaye anatamba na vibao vyake kama vile ‘msela jela, Maria na ******** lakini kikubwa ambacho kinawaweka roho juu mashabiki wa msanii huyu ni kitendo cha yeye kutotoka na alba yake ambayo inasubiriwa kwa hamu kubwa sana.

Inasemekana kuwa mchizi hakuwa ameridhika na kiasi cha fedha ambacho alitakiwa kukipata mara atakapowakabidhi wadosi master yake, jambo ambalo ni nadra sana kwa wasanii hasa wa muziki wa bongo fleva kuwa na msimamo wa aina hii, lakini mchizi amekomaa na alipoona miyeyusho akala kona.

Bushoke ambaye kwa sasa yuko nchini Afrika kusini ambako anaishi baa yake mzee Max Milian Bushoke, haijulikani kama ndio amefuata nyayo za mkongwe hayati Mbaraka mwinshehe ambaye baada ya kuona anazinguliwa na wadau kuhusu mauzo ya albam yake alikimbilia nchini Kenya ambako alianza upya kazi akiwa kama raia wa huko mpaka alipofariki.

Mpaka sasa bado haijajulikana lengo la kijana huyu kutimkia pande za kwa Mbeki, huenda naye ni kwenda kuanza moja au laah, maana alichowaambia wadosi kuhusiana na utaratibu ambao angeridhika nao, ni yeye kubaki na nakala halisi ya albam yake, kisha kila watakapohitaji kugonga kopi kwa ajili ya kuziingiza sokoni wanamuita na kumwambia idadi ya kopi kisha yeye atimue na nakala yake halisi, hapo ndio ngoma ikawa ngumu hivyo mchizi akaona mchongo sio, akaamua zake kula kona.

Inkuwa ngumu sana kwa wasambazaji na wauzaji wa kazi za wasanii wetu hapa nchini kuficha rekodi za mauzo, jambo ambalo kwa mtoni ni sifa kuweka hadharani juu ya mauzo ya kazi za wasanii wetu.

Source: Bongo5

{mos_sb_discuss:6}


Bongo5.com brings you the latest news from East Africa at your finger tips. If you have a story you’d like to share please send an email to [email protected]

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents