Burudani

Busu la Rihanna kwa Chris Brown kwenye VMA lamchefua Karrueche


Watu wengi walishangaa kuona wapenzi wa zamani Rihanna na Chris Brown kupigana busu na kukumbatiana kwenye ukumbi wa Staples Center juzi wakati wa MTV Video Music Awards jijini Los Angeles.

Lakini aliyeshangaa na kuumia zaidi si mwingine zaidi ya mpenzi wake wa sasa na Chris Brown, Karrueche Tran.

Chanzo kimoja kimeuambia mtandao wa US Magazine kuwa model huyo mwenye miaka 23 alichukia sana baada Chris kumpongeza Rihanna kwa kushinda kipengele cha Video of the Year kwa kuonesha hadharani kuwa bado anampenda.

“She felt the kiss was a public slap in the face,” kilisema chanzo hicho.

Kuonesha kuwa kitendo hicho juzi kupitia mtandao wa Instagram, Karrueche aliweka picha yenye maneno yasemayo,


‘Treat Your Girl Right’.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents