Habari

Bwana harusi achezea kichapo siku yake ya Ndoa, ajificha uvunguni mwa gari huku akiomba msaada (+Video)

Bwana harusi alitimuliwa katika harusi yake na umati wa watu uliokua na jaziba -baada ya mke wake wa kwanza kuwasili harusini kumfahamisha Bibi harusi kuwa mume anayemuoa alikua ameoa zaidi ya mke mmoja na kwamba ana wake wawili.

Asif Rafiq Siddiqi, ambaye alielezewa kama mwanaume mwenye ndevu mnene wa miaka zaidi ya 30, alisukumwa na kuzabwa makofi na umati wa watu hadi shati yake ilichanika wakati wa ghasia hizo baada ya kufichuliwa kuwa alikua ana wake wawili.

Bwana harusi alilazimika kujificha chini ya basi na baadae kuokolewa na watu wasiojulikana. Kuoa mke zaidi ya mmoja inakubalika kisheria nchini Pakistan.

Hata hivyo licha ya kwamba mwanamume anaweza kuoa hadi wake wanne, ni lazima apate idhini ya wake zake wa kwanza kabla ya kuoa tena.

Χαμός σε γάμο στο Πακιστάν: Αποκαλύφθηκε ότι ήταν παντρεμένος άλλες δύο φορές

Ilibainika kuwa Bwana Siddiqi alishindwa kutimiza hilo, na Bibi harusi na familia yake walifahamu juu ya ndoa zake za awali pale mke wa kwanza alipoingia kwenye ukumbi wa harusi iliyokua ikifanyika katika mji wa mwambao wa Karachi ambako sherehe zilikua zimepamba moto.

“Kuna tatizo gani dada?” mmoja wa ndugu wa Bibi harusi alisikika akiuliza katika video ya tukio hilo liliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

Mwanamke , Madiha Siddiqi, hakupoteza muda wa kuelezea kilichomleta ukumbini. “Ni mume wangu, ni baba wa mtoto huyu. Aliniambia anakwenda Hyderabad kwa siku tatu,” alisema mwanamke huyo ambaye alikua amemshikilia mtoto mdogo wa kiume aliyedai ni mtoto wao.Harusi ilivurugwa na mwanamke aliyedai ni mke wa kwanza kati ya wake watatu

Harusi ilivurugwa na mwanamke aliyedai ni mke wa kwanza kati ya wake watatu

Baada ya hapo familia ilijaribu kumpeleka katika chumba cha pembeni , jambo ambalo lilimpatia fursa ya kuwataja watu ambao alidai walikua ni ndugu zake.

“Yule ni mamamkwe wangu na yule ni jethani [wifi yangu], ambaye alisema kuwa mama yake alikua ni mgonjwa kwa siku tatu na alikua amewekewa drip ,” BIi Siddqi alielekea moja kwa moja hadi kwa Bibiharusi (mke mpya) na kumweleza kuwa asifikiri yeyey ni mke wa kwanza

“Hukujua kuwa alikua ni mme wangu? Hata hakufikiria juu ya mtoto huyo ambaye hana hatia.”

hata hivyo, haikuishia hapo: Bi Siddiqi alisema kuwa aliolewa na Bwanaharusi mwaka, baada ya kukutana nae katika Chuo kikuu cha Federal Urdu University, ambako Bwana Siddiqi anafanyia kazi.

Image result for Asif Rafiq Siddiqi beaten in his marriage

Halafu akafichua kuwa alioa mke wa pili kwa siri, anayeitwa Zehra Ashraf, ambaye ni mwalimu katika Chuo Kikuu cha Wanawake cha Jinnah kilichopo mjini Karachi, mnamo mwaka 2018.

Kwanza Bi Siddiqi alijua juu ya ndoa hiyo na aligundua kupitia ujumbe ambao aliupata kutoka kwa mke mpya wa mumewe. Siddiqi alisema kuwa Bwana Siddiqi awali alikana kuwa ana mke mpya, lakini baadae alikiri alikua amemuoa mke wa pili.

Ilikua ni Bi Ashraf ambaye pia alimfahamisha Bi Siddiqi kuhusu harusi ya hivi karibuni.

Haijawa wazi ni nini kilichotokea baadae. Hata hivyo polisi walioitwa kwenye eneo hilo wameiambia BBC kwamba ndugu wa Bibiharusi walimvamia na kumpiga Asif, wakachana ngua zake na kumpiga kipigo cha kila aina.

Maafisa walimuokoa Bwana Saddiqi, na kumpeleka kwenye kituo cha polisi cha karibu-lakini ndugu wa Bibiharusi walimfuata na kumsubiri ajitokeze.

Alipotokea tena walimvamia na kumlazimisha kukimbilia chini ya basi. Katika video ya tukio hilo, sauti zilisikika zikimtishia ”atoke chini ya basi au walichome”.

Kwa uoga, aliwajibu kwa sauti ya juu akisema “Subirini dakika moja, dakika moja “, huku akitambaa kutoka chini ya basi. Alipotoka baadhi ya watu waliingilia kati kuzuwia ghasia.

BBC ilijaribu kuwasiliana na Bwana Siddiqi na ndugu wa mke wake mpya kupata kauli zao, lakini hawakupatikana.

Rao Nazim, Mkuu wa kituo cha polisi cha Taimuriha aliiambia BBC kuwa hakukua na malalamiko rasmi yaliyo sajiliwa juu ya kisa hicho.

” Ni suala la kifamilia, na walalamikaji wanatakiwa kwenda kwenye mahakama ya familia kusuluhisha matatizo yao ,” alisema.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents