Burudani ya Michezo Live

Bwana Misosi adai umri ni chanzo cha wasanii wa zamani ‘kugaragazwa’ na wasanii wapya

Hitmaker wa Nitoke Vipi, Kipusa na Mungu Yuko Busy, Bwana Misosi amesema chanzo cha wasanii wengi wa zamani kupotea kwenye muziki, ni umri wao kuwa mkubwa.

1000763_487893981286269_1532873059_n

Akiongea na kipindi cha Kali za Bomba cha Bomba FM, Misosi alisema wasanii wengi wa zamani wana familia na hivyo kuwafanya watumie muda mwingi kufanya mambo mengi ya kuwaingizia kipato.

“Wengine wana majukumu, wengine wana wake, wana watoto, wengine wana Plan B zaidi, hata mimi nina Plan B, mimi ni mjasiriamali, mimi ni fundi umeme, lakini pia nina biashara zangu nafanya mbali na muziki,” alisema.

Hata hivyo, aliongeza pia kuwa wasanii wa siku hizi wamekosa ubunifu na wanachofanya ni kuigana zaidi.

“Madogo wa sasa hivi wengine wamekosa ubunifu, wanaigana, siongelei kwa ubaya,” alisema Misosi na kuongeza kuwa tangia ameanza muziki hadi leo yeye amekuwa na utambulisho wake peke yake na hafanani na mtu mwingine.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW