Promotion

Bye Bye Wema Sepetu

Wema SepetuHaya sasa ule wakati wa Miss Tanzania wetu Wema Sepetu kuachia ngazi umekaribia baada ya warembo ambao wapo kambini hivi tayari kwenda kuwadhihirishia watanzania kuwa nao wana uwezo wa kulitwaa taji

Wema Sepetu

 

Haya sasa ule wakati wa Miss Tanzania wetu Wema Sepetu kuachia ngazi umekaribia baada ya warembo ambao wapo kambini hivi tayari kwenda kuwadhihirishia watanzania kuwa nao wana uwezo wa kulitwaa taji la Miss World ambalo kutokana na kuwa hakuna ambaye anaamini atalikosa taji la Vodacom Miss Tanzania 2007.

 

Kinyang’anyiro hicho kinachotarajiwa kufanyika katika viwanja vya Leadesr Club maeneo ya kinondoni, itakuwa ni mara ya 13 tangu serikali iruhusu kufanyika kwa mashindano haya kwa mara nyingine tena hapa nchini tangu mwaka 1994 baada ya kufungiwa mwaka 1964.

 

Akizungumza na Bongo5 Miss Tanzania 2006 Wema Sepetu alisema “nakiri kuwa kwa mwaka huu majaji watakuwa na kazi kubwa ya kumchagua mshindi kwani Mamiss wa safari wote ni moto wa kuotea mbali ukizingatia watoto ni wakali ile mbaya”

 

Zawadi ambayo atajinyakulia mshindi wa shindano hilo la Vodacom Miss Tanzania 2007 ni gari aina ya RAV 4 yenye thamani ya shilingi milioni 45 itakayoambatana na kitita cha shilingi milioni 8, wakati mshindi wa pili atachukua fedha tasilimu shilingi milioni 5 na wa tatu shilingi milioni 3.5 wa nne shilingi milioni 2.5 na wa tano shilingi milioni 2.

 

Washindi kuanzia nafasi ya sita hadi ya kumi kila mmoja atapatiwa kifuta jasho cha shilingi milioni 1.2 wakati ambao hawatafika katika hatua hiyo watapozwa na shilingi laki sita kila mmoja.

 

Wema ambaye ni mmoja wa walimu katika kambi ya washiriki hao “washiriki wote wana vigezo na uwezo wa hali ya juu tofauti na mwaka jana sema watakachozidiana ni mbinu za kiubunifu ambazo yoyote anaweza kuzitumia na kuibuka mshindi”-Wema Sepetu.

 

Washiriki wa VodaCom Miss Tanzania 2007 ni Gladness, Queen David, Marietha Richard, ElizaBeth Mahuna, Perpetua George, Neema Khatibu, Anastazia Tanja, Ceprice Joseph, Imaculata Ngereza, Latifah Warioba, Baby Lema, Sada Hashim, Sofia Mwanyika, Fatma Kisoki, Monica John, Neema Chande, Cecilia Charles, Wahida Sylvester, Victoria Martin, Richa Adhia, Lilian Abraham, Irene Shirima na Eva Mbando.

 

Taji atakalovalishwa mshindi wa siku hiyo limetolewa na kampuni ya Tanzania One likiwa lina thamani ya shilingi milioni 28 huku likiwa limerembwa na madini aina Tanzanite.

 

Mwisho Wema alisema kushauri kwa Miss Tanzania atakayemrithi kuwa asisikilize maneno ya watu ambao watakuwa hawakuufurahia ushindi wake wala aiumizwe na habari za magazeti ya udaku kwani vyote ni vitu ambavyo vinaweza kukujenga au kukushushia hadhi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents