Michezo

CAF kuzihukumu Yanga SC na Simba SC leo

Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afriaka (CAF) lipo katika mchakato wa kupanga hatua ya awali  ya michuano ya kimataifa ngazi ya klabu ambapo Tanzania ikiwakilishwa na Yanga SC na Simba SC droo inayofanyika Jijini Cairo Misri.

Yanga SC na Simba SC zitaiwakilisha nchi katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika na Kombe la Shirikisho inayoandaliwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF).

Yanga itashiriki katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika hii ni baada ya kuwa bingwa ligi Kuu Tanzania Bara.

Wakati hasimu wake Simba SC wakisubiri kufahamu wataanza nanani katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika akiipata nafasi hiyo baada ya kutwaa Kombe la Azam Sport FederationCup(ASFC).

Michuano ya Caf inatarajia kuanza kutimua vumbi kuanzia Februari mwakani huku kamati kuu ya utendaji ya CAF ikiwa tayari imeshaanza vikao vyake tangu Desemba 11 ikijadili namna ya kuboresha michuano hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents