Michezo

CAF yabadili mfumo mzima wa michuano ya mataifa bingwa Afrika

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limesogeza mbele michuano ya kombe la mataifa bingwa Afrika mwaka 2019 kufanyika mwezi Juni na Julai badala ya Januari na Februari kama ilivyozoeleka.

Mabadiliko hayo yamefanywa ili kuepusha migongano ambayo hujitokeza mara kwa mara kwa vilabu vya Ulaya ambavyo hulazimika kuwatoa wachezaji katikati ya msimu.

Shirikisho hilo pia limeongeza idadi ya timu zitakazo shiriki michuano hiyo itakayo fanyika nchini Cameroon mwaka 2019 kufikia 24 badala ya 16 kama zilivyokuwa hapo awali. Mabadiliko hayo yalitiwa saini na kamati kuu ya CAF katika mkutano uliofanyika mji mkuu wa Rabat.

By Hamza fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents