Michezo

CAF yabadili mfumo wa ligi Zanzibar

Chama cha soka visiwani Zanzibar (ZFA) kupitia kamati yake ya utendaji imekutana leo kujadili masuala kadhaa ikiwemo namna yakupatikana kwa mfumo madhubuti utakaotumika kuendesha ligi kuu ya Zanzibar.

Hili linakuja baada ya mfumo uliopitishwa na klabu za kisiwani Pemba ambao uliwekwa baada ya Zanziabar kupatiwa uanachama wa kudumu CAF lakini kutokana na taarifa za kutolewa katika nafasi hiyo imeona umuhimu wa kukutana tena na wadau wa soka kutafuta njia mbadala.

Mara baada ya kukamilika kwa kikao hicho msemaji wa ZFA, Ali Bakar amesema kuwa kamati imependekeza kukutana na klabu zote ili kupanga mfumo mpya utakaotumika kwa ajili ya msimu ujao wa ligi.

Bakar ameongezakuwa kamati hiyo pia imezungumzia uhamisho huku ikizitaka klabu kulipia ada ya uanachama kwa ramjisi,ada ya mwaka wilayani, sambamba na ada ya mashindano huku akisisitiza kuwa timu itakayoshindwa kufanya hayo haitashiriki msimu ujao.

By Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents