Uncategorized

Caf yakanusha taarifa za kunyimwa visa Rais Ahmad Ahmad kuingia Marekani, ili kushiriki mkutano wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika (Caf), kupitia tovuti yake limesema kuwa limeshangazwa na habari iliyoenezwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii kuwa Rais Ahmad Ahmad amenyimwa visa ya kuingia nchini Marekani kushiriki mkutano wa Shirikisho la soka duniani FIFA unaonza kufanyika Machi 15 mwaka 2019 huko Miami.

Caf imesema kuwa imeshangazwa na kuvumishwa kwa habari hizo za uongo pasipo kutaka kuthibitisha ukweli.

Hata hivyo shirikisho hilo lenye dhamana ya kusimamia maendeleo ya soka la bara la Afrika limewathibitishia wanafamilia kandanda katika bara hili kuwa hakuna wakati wowote umewahi kutokea kwa Rais Ahmad Ahmad kunyimwa visa ya kuingia Marekani.

Huku likisema kuwa Rais huyo ni kama wanachama wengine wa FIFA, visa yake hushukhulikiwa na kutolewa na ubalozi wa Marekani nchini Misri.

Na kuongeza kuwa Rais hueshimu sheria na taratibu zote za upatikanaji wa visa, na hukubaliana na kanuni za kila nchi.

Kwa taarifa hiyo ya Caf inaonyesha dhahiri kuwa mpaka sasa Rais Ahmad Ahmad hajapata visa na sababu za msingi kuchelewa kwa viza hiyo hazijatolewa.

Image result for ahmad ahmad

Mapema hapo jana kuzuka kwa taarifa kutoka kwenye vyombo mbalimbali vya habari vya Kimataifa pamoja na mitandao ya kijamii kuwa Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (Caf), Ahmad Ahmad amenyimwa visa ya kuingia Marekani alikotakiwa kuhudhuria kikao cha Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).

Miongoni mwa mada zinazokwenda kujadiliwa jijini Miami nchini Marekani kwenye mkutano huo wa FIFA ni pamoja na mashindano ya kombe la dunia la mwaka 2022 na mabadiliko makubwa ya michuano hiyo.

Rais wa Caf Ahmad Ahmad alichaguliwa kwenye uchaguzi uliyofanyika mwaka 2017 baada ya uongozi wa juu wa shirikisho hilo la soka kugubikwa na rushwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents