Michezo

Caf yamuweka chungu kimoja Mbwana Samatta na mkali wa Chelsea, Didier Drogba

Shirikisho la soka Barani Afrika Caf, limemtaja mshambuliaji hatari wa Taifa Stars ya Tanzania na klabu ya Aston Villa kutoka pale Premier League, Mbwana Samatta kuwa ni mingoni mwa wachezaji wanne kutoka Afrika wenye uwezo wa hali ya juu kabisa katika matumizi ya vichwa wawapo uwanjani.

 

Caf imesema kuwa Afrika imebahatika kushuhudia wapiga vichwa wazuri kunako soka, baadhi ya hao ni pamoja na aliyekuwa mshambuliaji wa klabu ya Chelsea na timu ya taifa ya Ivory Coast, Didier Drogba.

Flávio da Silva Amado ambaye alikuwa striker wa timu ya taifa ya Angola na klabu ya Atlético Petróleos de Luanda kutoka huko huko, huku Caf ikimtaja wa nne kuwa ni Mfarao, Hossam Hassan mkali huyu wa zamani wa klabu ya Zamalek.

Samatta header afunga Goli la Kihistoria Carabao Cup Aston villa ...

Shirikisho hilo lenye dhamana ya kusimamia maendeleo ya soka Barani Afrika limemuweka Mbwana Samatta nafasi ya pili kwa uwezo wake wa kutumia mipira ya vichwa baada ya Didier Drogba waliyemuandika kama mchezaji wa kwanza.

Aston Villa 1-2 Manchester City - PLAYER RATINGS: Carabao Cup ...

Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa vya habari, Samatta ambaye kwa sasa anasakata kabumbu la kulipwa kunako ligi pendwa zaidi duniani Premier League ana jumla ya magoli 31 aliyofunga kwa kutumia kichwa.

Mbwana Samatta amejiunga na klabu ya Aston Villa ya England kwa dau la paundi milioni 10 ikiwa ni mkataba wa miaka minne na nusu akitokea KRC Genk ya Ubelgiji.

Mtanzania huyo pekee aliyepata nafasi ya kucheza Premier League, ametua Villa baada ya kufunga jumla ya magoli 43 kwenye michezo 98 aliyocheza kwenye ligi ya Ubelgiji akiwa dani ya kikosi cha Genk licha ya kusumbuliwa na majeraha.

Imeandikwa na Hamza Fumo

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents