DStv Inogilee!

CAF yataja waamuzi hawa kusimamia mechi ya Yanga SC dhidi ya Gor Mahia

Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Africa CAF limetaja waamuzi kutoka nchini Somalia kuchezesha mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya makundi kati ya Gor Mahia ya Kenya na Young Africans ya Tanzania utakaochezwa Uwanja wa Moi Kasarani Julai 18,2018.

Kwenye mchezo huo Mwamuzi wa katikati atakua Hassan Mohamed Hagi akisaidiwa na Mwamuzi namba moja Hamza Hagi Abdi, Mwamuzi msaidizi namba mbili Suleiman Bashir Sh.Abdi na Mwamuzi wa akiba Nur Muhidin Mohamed.

Mtathmini waamuzi anatokea Gabon Jan Olivier Mbera na Kamishna wa mchezo anatokea Africa Kusini Simphiwe Brian Xaba sambamba na mratibu wa mchezo huo Nomsa Jacobeth Mahlangu.

Aidha mchezo wa marudiano kwa timu hizo utakaochezwa July 29,2018 Kwenye Uwanja wa Taifa wenyewe utachezeshwa na Waamuzi kutoka Mauritius.
Mwamuzi wa katikati atakuwa Ahmed Imtehaz Heeralall akisaidiwa na Mwamuzi msaidizi namba moja Cauvelet Louis Ralph Fabian,Mwamuzi msaidizi namba mbili Akhtar Nawaz Rossaye na Mwamuzi wa akiba Ganesh Chutooree.

Kamishna wa mchezo anatokea Zambia Patrick Kangwa, Mtathmini waamuzi anatokea Congo Louzaye Rene Daniel wakati Mratibu anatokea Nigeria Nasiru Sarkintudu Jibril.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW