Habari

CAG atoa neno kuhusu deni la Taifa

Serikali imesema kuwa Deni la Taifa limeendela kuwa stahimilivu hali inayoonyesha kuendelea kuimarika kwa uchumi wa Taifa letu.


Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Assad

Akizungumza na waandishi wa habari,mjini Dodoma Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG ) Prof. Mussa Juma Assad amesema kuwa hadi kufikia tarehe 30 June 2017 deni la taifa lilikuwa trilioni 46.08 ambapo deni la nje ni Shilingi Trilioni 32.7 sawa na asilimia 71 na deni la ndani ni Shilingi Trilioni 13.34 sawa na asilimia 29.

Akifafanua amesema kuwa matokeo ya ukaguzi huo yatawekwa wazi mara baada ya ripoti husika kuwasilishwa rasmi Bungeni kabla ya tarehe 12, April 2018 na baada ya hapo nakala ngumu za vitabu zitapatikana kwenye Ofisi zote za Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali na kwenye tovuti (www.nao.go.tz).

Kwa mujibu wa Ibara ya 143 (4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 (iliyorekebishwa mwaka 2005), mnamo Machi 27, 2018 Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Juma Assad aliwasilisha ripoti ya ukaguzi wake kwa mwaka wa fedha unaoishia June 2017 kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents