Michezo

Cameroon uso kwa uso na Algeria kuwania tiketi kucheza kombe la dunia 2018

Duru la pili la makundi ya kuwania tiketi za kufuzu kushiriki kombe la dunia hapo mwakani nchini Urusi linatarajiwa kuendelea tena mwezi Octoba wakati kwa upande wa Afrika vitakali itakuwa ni mchezo kati ya timu ya taifa ya Cameroon itakayo wavaa wa Algeria.

Mchezo wa Cameroon dhidi ya Alageria unatarajiwa kupigwa Octoba 7 wakati ambapo michezo mingine ikichezwa katika viwanja tofauti barani Afrika.

Timu ya taifa ya Guinea ikijitupa uwanjani kuvaana na Tunisia wakati Libya ikicheza na DR Kongo wakati siku hiyo ya tarehe 7 ya mwezi Octoba Nigeria ikiwa uwanjani dhidi ya Zambia.

Michezo mingine itakayopigwa mapema kwa Afrika ni Octoba 6, wakati Mali dhidi ya Ivori Coast, Morocco na Gabon, Afrika Kusini dhidi ya Burkinafaso huku Caper Verde ikicheza na Senegal.

Sweeden itaikabili Luxermburg, Oustria watachuana na Serbia, Uturuki dhidi ya Iceland, Italia ikutana na Macedonia, Hispania dhidi ya Albania, Montenegro na Dernmark, Moldova dhidi ya Wels, Ujerumani na Ireland ya Kaskazini na Uingereza watakutana na Slovenia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents