Canavaro, Nizar njia panda canada

Canavaro, Nizar njia panda canada
Nyota wa nne wa Tanzania wameshindwa kujiunga na mabingwa wa Canada,
Vancouver Whitecaps baada ya kukosa viza ya kuingia nchi hiyo

Wachezaji hao waliokwama ni Nadir Haroub"Canavaro" kutoka Yanga, Nizar
Khalfan (Moro United), Zahoro Pazi (Mtibwa Sugar ) na chupikizi Abdul
Deen kutoka mkoa wa Kagera.

Msemaji wa LZ Enterprises alisema jana kuwa wachezaji hao wanne
walitakiwa kuondoka nchi baada ya mechi ya kirafiki ya kimataifa kati
ya Taifa Stars na New Zealand.

Afisa huyo alisema wachezaji hao wameshinda kupata viza hapa na
kulazimika kwenda nao Nairobi, Kenya kwa ajili ya kufanikisha jambo
hilo.

Alisema kwa mujibu wa ratiba ya klabu ya Whitecaps, wachezaji hao
walitakiwa kuungana na timu hiyo kuanzia leo (Juni 8) kwa ajili ya
majaribio, lakini tayari wameshatumia taarifa kuhusu tatizo hilo.

Msemaji huyo ambaye hakupenda jina lake litajwa alisema wachezaji hao
wamerudi nchini wataambia kuhusu viza zao kukamilika Alhamisi ijayo.

"Baada ya wiki moja nitakuwa kwenye nafasi nzuri ya kusema ni lini
wachezajia hawa watajiunga na timu hiyo, tutabidi kusubili kwa wiki
moja kujua kama tumerusiwa kuondoka," alisema.

Tumeshawaeleza Vancouver kuhusu ili tatizo wametuambia tusiwe na shaka
bado wanawasubili kufanya majaribo chini ya benchi la ufundi.

Kwa mujibu wa afisa huyo alisema hakuna tatizo lolote kuhusu wachezaji hao kupewa ruhusa na klabu zao juu ya safari hiyo.

Wakati huo huo Vicky Kimaro anaripoti kuwa; Uongozi wa klabu ya Yanga
umeweka baya majini ya wachezaji wake waliotimukia Ulaya na kuziomba
timu walizoenda kujiunga nao kufutwa utaratibu wa usajili wao.

Katibu mkuu wa Yanga, Lucas Kisasa alisema wamepokea maombi kuombewa
kibari kwa mchezaji wake Shadrack Nsajigwa kubaki nchini Ufaransa.

Huku uongozi huo wa Yanga ukitaka klabu iliyomchukua mchezaji wake Credo Mwaipopo ya nchi Sweden kufutwa taratibu za uhamisho.

Credo ni mchezaji wetu anamkataba nasi wa miaka miwili, hata safari
yake ya kwenda Sweden alitoroka hivyo ni vizuri kwa klabu iliyomchua
kufutwa utaratibu wa kumsajili kwa njia sahihi.

Naye kiungo Castro Mumbala imedaiwa kuamejiunga na klabu ya African Lyon kwa ajili ya msimu ujao wa ligi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents