Aisee DSTV!

Cardi B aahirisha show yake iliyouza tiketi 5000, Yadaiwa upasuaji wa kupunguza tumbo na kifua wamuendea vibaya

Waandaaji wa tamasha la Spring Bling, wamelazimika kutangaza kuahirishwa kwa show ya Cardi B iliyopangwa kufanyika leo usiku Mei 24 na badala yake itafanyika Septemba 8 mwaka huu.

Cardi B

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, umeeleza kuwa sababu za kuahirishwa show hiyo, Ni kutokana na upasuaji mdogo aliofanyiwa Cardi B wa kupunguza nyama uzembe tumboni na kifua kutokwenda vizuri.

Cardi B wiki moja iliyopita iliripotiwa kuwa amefanyiwa upasuaji mdogo wa kupunguza nyama uzembe tumboni, hii ni baada ya tarehe 5 Mwezi Mei mwaka huu kutangaza kuwa atakuwa tayari kusogeza tarehe za show zake zote ili kufanyiwa upasuaji.

Show ilitarajiwa kufanyika leo Mei 24 usiku katika ukumbi wa  92Q mjini Baltimore na tayari tiketi 5000 zimeshanunuliwa mpaka sasa.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW