AFCON 2019 Tupogo!
Vodacom Data Datani!

Cardi B amjibu Nicki Minaj kwa staili ya aina yake

Cardi B amjibu Nicki Minaj kwa staili ya aina yake

Rapper wa kike kutoka Marekani Belcalis Marlenis Almanzar a.k.a Cardi B ameamua kumjibu mpinzani wake mkubwa kwa sasa Nicki Minaj kwa staili ya aina yake kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Kabla ya drama hizi kuendelea hawa madada wawili kutoka Marekani walianza vizuri kufanya muziki lakini maigizo yalianza pale waliposhirikishwa katika nyimbo moja na kundi la muziki kutoka nchini humo linalojulikana kama Migos katika nyimbo yao ya Motorsports.

Baada ya maigizo hayo kuendelea Nicki alikuja kuongea katika vyombo vya habari na kudhibitisha kuwa hana ugomvi na Cardi B na kumpongeza kwa mafanikio yake makubwa aliyoyapa kupitia muziki wake,lakini alipoulizwa Cardi B hakuonesha kufurahishwa na maneno hayo ya Nicki.

Baada ya Cardi B kujifungua mtoto wake alianza vibwanga kwani alianza kupost video zinazoonesha akimponda msanii flani ambaye hakuweza kumtaja jina na siku ya maadhimisho ya mitindo yanayofanyika kila wiki katika jiji la New York zinazojulikana kama Harper Bazaar ICONS ambapo ugomvi ulitokea mkubwa hadi Cardi B kumrushia Nicki viatu.

Pia katika mahojiano aliyoyafanya Nicki na kusema “Tukio hilo lilikuwa la udhalilishaji kwa sisi wote wawili,siwezi kuzungumzia malezi ya mtu inanishangaza jinsi watu wanavyopenda kunifanya mimi ndio nionekane mbaya mmeona ile video iliyovuja lakini mimi ntaonekana mpumbavu”

NEW YORK, NY – OCTOBER 30: Cardi B attends BACARDI presents Dress To Be Free with performances by Cardi B and Les Twins at House of Yes on October 30, 2017 in New York City. (Photo by Michael Loccisano/Getty Images)

Nicki aliongeza ” Mwanamke huwezi kumuachia mwanaume kama mwenyewe hataki,una hasira na nani ? aliuliza Nicki Umenikuta kwenye muziki sijawahi kutembea na DJ ili wapige ngoma zangu”

Baada ya mahojiano hayo ya Nicki kuhusu kumzungumzia Cardi B kuwa amewahi kutembea na DJ ili apigiwe ngoma zake hivyo Cardi B anabebwa basi Cardi wiki hii na yeye kaamsha mambo baada ya kujibu mapigo kwa kupost orodha ya wasanii waliouza albam zao kwa wingi zaidi mwaka 2018 huku katika orodha hiyo hakuiweka albam ya Nicki Minaj ya ‘Invasion Of Privacy’ na queen ” huku akiandika chini ya post hiyo kuwa ” Number dont fuckin lie” yaani Namba haidanganyi.

 

By Ally Juma

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW