DStv Inogilee!

Cardi B atangaza kuachana na mpenzi wake Offset ‘tutakuwa marafiki tu, mapenzi na yeye basi’

Rapper Cardi B ametangaza rasmi kutemana na mpenzi wake, Offset ambaye walifunga ndoa ya kimya kimya mwaka mmoja uliopita.

Image result for cardi b and offset
Offset na Cardi B

Cardi B ndiye wa kwanza kutangaza taarifa hizo kupitia video yake aliyoiposti kwenye ukurasa wa Instagram, ambapo amesema “Kila mtu amekuwa akiulizia hali iliyvyo kwa sasa, lakini ukweli ni kwamba nimehangaika hadi dakika ya mwisho, kuhusu mzazi mwenzangu ambaye kiukweli ni rafiki yangu hata kibiashara lakini mambo hayaendi sawa. Huyu ni mtu ambaye ninamtegemea kila ninapopatwa na tatizo amekuwa kimbilio, tumependana kweli lakini mambo hayajaenda sawa, tumepambana kwa muda mrefu lakini penzi letu linayumba hatuelewani, mimi na yeye tutabaki kuwa marafiki kwani ni baba wa mtoto wangu.“.

Cardi B na Offset wamedumu kwenye mapenzi kwa miaka miwili na wamefanikiwa kupata mtoto mmoja aitwaye Kulture Kiari Cephus.

 

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW