Shinda na SIM Account

Caribbean yapigwa na kimbunga kingine kikubwa

Kisiwa cha Caribbean kimeendelea kukumbwa na jinamizi la kipunga katika eneo lake la Dominica.

Kimbunga kiitwacho Maria kilichotajwa kuwa na nguvu ya kiwango cha tano na upepo wa kasi ya kilomita 160 kwa saa, kimeharibu tena kisiwa hicho Jumatatu hii.

Kimbunga hicho pia kimeharibu mpaka nyumba ya waziri mkuu Roosevelt Skerrit. Kupitia mtandao wa Facebook Waziri huyo ameandika, “My roof is gone. I am at the complete mercy of the hurricane. House is flooding.”

Wakati huo huo uwanja wa ndege wa Dominica na bandari iliyopo eneo hilo vimefungwa. Kimbunga hicho cha Maria kinatajwa kupita sehemu ambazo kimbunga cha Irma chenye ukubwa wa kiwango cha tano kilipita wiki mbili zilizopita.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW