Habari

CARLIFONIA: Moto waunguza zaidi ya Ekari 100000, Trump ajibizana na gavana mitandaoni – Video

CARLIFONIA: Moto waunguza zaidi ya Ekari 100000, Trump ajibizana na gavana mitandaoni - Video

Rais wa Mamerika, Donald Trump ametishia kupunguza fedha za ufadhili kwa gavana wa jimbo la Carlifonia kutokana na milipuko ya moto unaoendelea kuenea California, Trump ameongea hayo kupitia Twitter yake.

Karibia ekari 100,000 zimeharibiwa na moto katika msitu uliopo Carlifonia katika wiki za hivi karibuni, na maelfu wamelazimishwa kutoka nyumba zao.

Bwana Trump alimlaumu gavana wa chama cha Democratic  Gavin Newsom, akisema kwamba wamefanya “kazi mbaya ya usimamizi wa pori hilo”.

“Kila mwaka, moto huwaka California ni kitu hicho hicho – halafu anakuja Serikalini na kuomba msaada Hakuna la zaidi. Bwana Newsom, ambaye amekosoa sana sera za mazingira za Bw Trump, alijibu: “Hauamini mabadiliko ya hali ya hewa. Umeachiliwa kutokana na mazungumzo haya.”

Inaelezwa kuwa ongezeko la joto duniani ndio umesababisha moto mkubwa California bila kujali mvua ilikuwa ya baridi kali, kulingana na utafiti uliochapishwa hivi karibuni katika Kitabu cha Sayansi ya Kitaifa ya Sayansi.

Hali ya joto husababisha kukausha kwa mimea na kusababisha moto kuwaka zaidi.

Rais alitoa tishio kama hilo la kukata kutoa misaada ya shirikisho mwaka jana, wakati moto mbaya zaidi katika historia ya California ulipouwa watu 86.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents