Michezo

Casillas amwaga machozi wakati akiwaaga mashabiki wa Real Madrid

Mashabiki wa Real Madrid jana waliagwa kwa majonzi na aliyekuwa golikipa na nahodha wao, Iker Casillas.

2A77842F00000578-3158074-image-a-59_1436701173742

Mlinda Mlango huyo ameaga rasmi tayari kuelekea Porto kuanza maisha mapya ya soka baada ya kudumu klabuni hapo kwa takribani miaka 25 akitokea timu ya vijana ya Real Madrid.

“Nimekuja katika uwanja huu ambao ni mkubwa kabisa kuwaaga ninyi nyote, hasa kwa mashabiki wa Madrid. Kuanzia leo (Jumamosi) sio mchezaji wa Madrid tena, nitakuwa mchezaji wa Porto,” ” alisema Casillas.

2A7764D000000578-3158074-image-a-55_1436699744306

“Naelekea Porto kutokana na sababu nyingi. Kwanza kabisa naenda kujiunga na Porto kwa sababu ya hamasa kubwa kutoka kwa kocha. Pili, kwa sababu ya mapenzi ya dhati juu yangu. Nitafanya kila niwezalo ili nisiwaangushe na kupambana kwa juhudi zangu zote kuhakikisha tunashinda makombe mengi kadri nitakavyoendelea kuwa pale.”

Akiongea kwa kusuasua, mlinda mlango huyo ambaye amewahi kushinda kombe la dunia akiwa na Uhispania, alitoa shukrani za dhati kwa mchango mkubwa ambao Madrid wamempa, huku pia akiwaeleza mashabiki kumkumbuka “kama mtu bora” na sio golikipa bora.

2A773F4600000578-3158074-image-a-42_1436697578534

“Klabu hii sio tu imenifundisha kuwa mwanamichezo, bali pia imenifundisha kuwa binadamu. Nimejifunza mengi sana kutoka kwa makocha wote waliowahi kupita hapa. wamekuwa ni sehemu muhimu sana katika maendeleo ya tasnia yangu ya soka. Kila siku tumekuwa tukiwa sehemu ya klabu hii na tumekuwa tukipata sapoti kubwa pia. Ninataka kusema asante sana kwa wazazi wangu na familia yangu kwa ujumla,” aliongeza.

“Asanteni sana mashabiki wote wa Madrid kwa sapoti yenu, mmenisaidia kutwaa kila kombe hapa, kila ushindi, kuwa pamoja nami katika wakati mgumu na mzuri niliokuwa nao. Kwa kunipa mkono pale nilipohitaji. Sihitaji kukumbukwa kama golikipa mzuri au golikipa mbaya, bali nataka kukumbukwa kama mtu mzuri, bila kujali mapungufu yangu. Asanteni. Maelfu ya asante kwenu. Popote nitakapokwenda, Nitasema kauli mbiu hii ya ‘Hala Madrid’. Natumaini kwa miaka michache ijayo tutaonana. Nasema kwaherini, sababu sio kwaheri. Natumaini tutaonana siku za hivi karibuni. Asanteni nyote.”

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents