Habari

Cassim awakumbusha waimbaji wa Bongo kuandika mashairi na sio kujiimbia tu

Hitmaker wa ‘I love You’, Cassim Mganga amewataka wasanii wenzie kuacha mtindo wa kutunga nyimbo zisizokuwa na mashairi.

Kassim-Mganga-serengeti-fiesta-Mbeya.

Akizungumza na Bongo5 hivi karibuni, Cassim, alisema wasanii wanatakiwa kufuata utaratibu wa kuandika mashairi ili kuzipa nyimbo uthamani na pia kuwafanya wadau kuvutiwa kuzisikiliza nyimbo kutokana na mpangilio wake mzuri.

“Nashangaa sana wasanii wanatunga nyimbo ambazo hazina mashairi, huu ni uzembe. Msanii anatakiwa kuhakikisha mashairi yanaeleweka ili kupata mtiririko mzuri unaoeleweka katika nyimbo zetu kwa sababu ni utaratibu ambao upo kwa nini tusiufuate,” alihoji msanii huyo.

Katika hatua nyingine, Cassim alisema wadau wasubiri kwa hamu kitu kipya kutoka kwake ambacho kitakuwa ni video ya hit yake hiyo iliyopo kwenye mchakato kwa sasa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents