Burudani

Cassper afunguka kuhusu bifu lake na AKA

Msani kutoka South Africa Cassper Nyovest kwa sasa yupo nchini Nigeria na anataka kila mtu ajue kuhusu hilo.Rapa huyo yupo Lagos kwa muda sasa toka tuzo za Soundcitymvp na ametweet kwa kusema kwamba hayuko tayari kuondoka jijini Lagos,Nigeria.

kukaa kwake katika jiji hilo limewafanya WaNigeria kujivunia jinsi wanavyoweza kuwahudumia wageni wao wa kimataifa.

Wakati akiwa katika mji huo, Alizungumza na waandishi wa habari ambako alifunguka juu ya ugomvi wake na AKA. Moja ya pointi muhimu Cassper aliyo sema ni kwamba hawezi kujifanya yupo sawa na kila mtu ili tu aweze kutengeneza kiki.
Cassper alionngelea tamasha alilolifanya decemba mwaka jana katika uwanja wa mpira uitwao FNB Stadium na aliweza kuuza tiketi zaidi ya 68000.

Cassper alisema katika mahojiano na kipindi cha THE BEAT kuwa alipigiwa simu na AKA siku chache kabla ya tamasha lake na AKA alimuambia kwamba wamalize bifu lao kwa yeye kwenda na kutumbuiza kwenye tamasha hilo na amlipe kiasi cha randi milioni moja. Cassper alimjibu AKA kwa kumuambia kuwa hajamuomba yeye kuja kwenye tamasha lake na kama ingekuwa ni kumaliza bifu lao basi angekuja kutoa msaada na sio kutaka kulipwa kiasi cha Randi milioni moja.

Cassper aliwaambia waandishi wa habari kuwa aliwalipa tu baadhi ya wanamuziki waliotumbuiza katika tamasha lake lakini wengi wao hawakutaka kulipwa na walifanya kama msaada tu.Waandishi walimuuliza ni kwanini alipendekeza hilo kwa AKA na Cassper alijibu kwa kusema “i am not about faking unity for the sake of hype.”

Cassper aliongezea kwa kusema kwamba “hakuna haja ya wao kujifanya kama wako sawa kwa ajili ya kutengeneza pesa kama ni pesa ndo anachokitaka basi tushindane mimi na yeye uwanjani kuliko kujifanya kama sisi ni washkaji.”

Rapa huyo kutoka Afrika kusini hakuishia hapo tu alisema pia “kama AKA alitaka kusaidia basi angenunua tiketi kama walivyo fanya wanamuziki wengine kama Black Coffee lakini yeye hakufanya hivyo alichokuwa anataka ni kutengeza kiki tu nasio kingine.”

Na Raheem Rajuu

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents