Burudani
Cassper Nyovest kutua Dar July
Cassper Nyovest hatarajii tu kuachia Album yake ifikapo Mei 7 ya mwaka huu yenye nyimbo 16 ndani yake, bali hata kutinga Dar na kukutana stage moja na Future kutokea Marekani.
Rapa huyo kutokea nchini South African atakutana pia na Diamond Platnumz wakishare stage moja ambapo watafanya show mwezi July mwaka huu.
Hii itakuwa mara ya pili kwa Future kutua Afrika ambapo awali alikuja kwenye Tuzo za MTV Africa Music Awards (MAMAs) mwaka jana 2016, ambako alifanya show kwenye stage moja na wakali kama vile : Yemi Alade, Ali Kiba , Emtee, Kwesta na Patoranking.
Na Laila Sued