Habari

CCM wafanya maajabu mengine mkoani Manyara, wagombea vyama vya upinzani waingia mitini

Wagombea wawili wa ubunge kwa tiketi ya CCM katika jimbo la Simanjiro na Babati Mjini mkoani Manyara wamepita bila kupingwa baada ya wagombea wa vyama vingine kutorejesha fomu siku ya jana.

Taarifa iliyotolewa jana Novemba 3, 2018 na Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro,  Yefred Myenzi imeeleza kuwa hadi saa 10 jioni jana hakuna mgombea aliyerudisha fomu zaidi ya mgombea wa CCM, James Millya hali iliyopelekea Mgombea huyo kupita bila kupingwa.

Kwa upande mwingine, Mkurugenzi wa mji wa Babati, Fortunatus Fwema naye amesema mgombea ubunge wa Babati Mjini kwa tiketi ya CCM, Pauline Gekul amekosa mpinzani baada ya Mgombea wa NRA, Feruzi Juma kuchukua fomu bila kuirejesha huku mgombea wa CUF, Abubakari Peter fomu yake ikionekana kuwa na mapungufu.

Wagombea wote wawili Gekul na Millya walikuwa wabunge wa majimbo hayo kwa tiketi ya CHADEMA na walijiuzulu kutoka chama hicho na kuhamia CCM.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents