Habari

CCM yaendeleza ubabe Monduli na Ukonga kwenye uchaguzi mdogo wa ubunge

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeendeleza ubabe kwenye chaguzi ndogo za majimbo ya Monduli na Ukonga kwa kufanikiwa kuyatwaa majimbo hayo.

Tokeo la picha la polepole na waitara
Mwita Waitara

Jimbo la Ukonga, mgombea wa Ubunge kwa tiketi ya CCM, Mwita Waitara ameshinda kwa kura 77,795 sawa na asilimia 89.1 huku akifuatiwa Asia Msangi wa CHADEMA kura 8,676 sawa na asimia 9. Hii kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa leo asubuhi na msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo, Jumanne Mashauri.

Matokeo mengine ni ya Jimbo la Monduli, ambapo CCM pia imeibuka kidedea kwa ushindi wa kura 65,714 kupitia kwa mgombea wake, Julius Kalanga akifuatiwa na Mgombea wa CHADEMA, Yonas Laizer aliyepata kura 3,183 .

Wagombea wote kwa tiketi ya CCM walioibuka kidedea, awali walikuwa wabunge wa CHADEMA kabla ya kuhamia CCM.

Mpaka sasa majimbo yote yaliyorudiwa uchaguzi CCM imeibuka kidedea kwa ushindi wa kishindo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents