Habari

CCM yampata mrithi wa Lazaro Nyalandu

Baada ya mchakato mrefu wa kura za maoni katika majimbo matatu yaliyokuwa yameachwa wazi likiwemo jimbo la Singida Kaskazini lililokuwa linashikiliwa Mhe. Lazaro Nyalandu, Hatimaye Chama cha Mapinduzi tayari kimetangaza majina matatu ya wagombea watakaosimama kuwania Ubunge kwenye majimbo hayo.

CCM imemsimamisha Monko Joseph kugombea jimbo la Singida Kaskazini ambalo liliachwa wazi na aliyekuwa mwanachama wao Lazaro Nyalandu.

Majina mengine ni Damas Ndumbaro jimbo la Songea Mjini, na Stephen Kiruswa jimbo la Longido.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu na Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Ndg Humphrey Polepole ameeleza kuwa wagombea hao kuanzia Kesho Desemba 16 wataanza kwenda kuchukua fomu NEC tayari kwa kujiandaa kwa uchaguzi mdogo.

Soma zaidi taarifa iliyotolewa na CCM;

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents