Habari

CCM yashangaa kauli hii ya Mh. Lowassa

By  | 

Chama cha Mapinduzi mkoa wa Arusha kimekanusha kauli ya aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa aliyesema wananchi wa Arusha wanasikitika kwa hatua ya kutuma mwakilishi kwenye msiba wa wanafunzi wa Lucky Vicent na vile vile Rais Magufuli kutokuhudhuria msiba huo wakati huo Rais Magufuli alimtuma Muwakilishi ambaye ni Bi Samia Suluhu.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Michael Lekule ,amesema kauli ya Waziri huyo mstaafu ameitoa kwa kudanganya wananchi na kuonesha serikali ya Magufuli haishirikiani na wananchi.

“Serikali ilijitoa kwa hali na mali kuwezesha familia 35 kwenda kupumzisha wapendwa wao,na ilihakikisha kila mwili unapumzika mahala popote familia inapopataka,tunajiuliza walitaka nini kama kote nafasi ilijazwa na serikali ya Magufuli,” alisema Lekule.

“CCM inakanusha kwanguvu upotoshaji huo,hata ukiangalia siku ile uwanja wa shekh Amri Abeid wanaccm walijaa uwanjani ,kikubwa CCM imeguswa na msiba uliotokea na Rais wetu amekuwa bega kwa bega juu ya tukio lililotokea,”amesema

Hivi Karibuni aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa aliongea na waandishi wa Habari kuwa Watu wa Arusha wamesikitika kutomuona Rais Magufuli katika msiba huo na kumtuma mwakilishi. Ndipo wananchama hao walipoamua kujibu.

Na Emmy Mwaipopo

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments