Habari

CCM yaweka wazi kupotea kwa Ndg. Kinana

Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa (CCM), Humphrey Polepole amesema kuwa Katibu mkuu wa chama hicho Abdulrahman Kinana alikuwa akiugulia afya yake pindi yupo kazini hivyo alichukua muda wa kutosha kwenda nje ya nchi kupatiwa matibabu.

Polepole alitoa kauli hiyo jana, alipokuwa akifanya majumuisho ya ziara yake iliyolenga kukagua uhai wa CCM mkoani Arusha.

“Lakini unapoona Katibu wetu Mkuu wa CCM anaulizwaulizwa yuko wapi na hata watu wasiokuwa wana CCM, hii inaonyesha kiwango cha imani cha Watanzania kinarejea kwa kasi kubwa, hasa katika kipindi hiki tunapofanya mageuzi makubwa ndani ya chama chetu.

“Na kwa hakika najua viongozi wa vyama vingine wasioonekana hawauliziwi na mtu yeyote, kwetu sisi ni dalili njema sana.Nipende tu kuwaambia jana nimeongea na Komrade Kinana bado yuko kwenye mapumziko ya kujitizama afya yake.Ninyi wote ni mashahidi mzee wetu huyu alifanya kazi kubwa ndani ya CCM na kwenye Serikali na pia kwenye wigo wa kimataifa, hasa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.”

“Tangu akiwa kwenye mkutano mkuu maalumu wa CCM Dodoma hakuwa sawa kiafya, alikuwa anafanya yote haya akiugulia afya yake kwahiyo ikakubalika achukue muda wakutosha wa kuitizama afya yake nje ya nchi na anapo rejea mgonjwa akitoka hospitali huwa hakimbii kazini, shambani moja kwa moja inashauriwa kitaalam atumie muda wa kupumzika ili kuimarisha afya yake na nimezungumza nae anaendelea vizuri yuko madhubuti kabisa kuliko jana,” alisema Polepole.

Katibu mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana hajaonekana hadharani kwa muda tangu Rais Magufuli aliposema kuwa yuko India.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents