Michezo

CECAFA yataja mwisho wa majina

 

Baraza la vyama soka  kwa nchi za Afrika Mashariki na kati (CECAFA) imetaja Novemba 22  kuwa siku ya mwisho ya kuwasiliana majina ya wachezaji wa timu zinazoshiriki mashindano ya Chalenji kwa mwaka huu.


Akizungumza na waandishi wa Habari kutoka Kenya, Ofisa habari wa CECAFA, Phin Muyeshi, alisema hadi sasa hakuna timu iliyowasilisha majina ya wachezaji watakao shiriki michuano hiyo.

Tayari tumeshazungumza na timu zote na tumezipa utaratibu wa kufuata.Tunaamini ziko kwenye maandalizi ya mwisho mwisho zikijiandaa na mashindano yajayo ya Chalenji”alisema Muyeshi.

Kwa kawaida nchi wakishiriki na waalikwa hutakiwa kuwasilisha majina mapema kuipa nafasi CECAFA kupanga utaratibu hasa wa usafiri wa kuzifikisha kwenye vituo vya mashindano.

Tanzania bara ndio wenyeji wa mashindano hayo mwaka huu na yatafanyika jijini Dar es salaam kuanzia Novemba 27 hadi Disemba 12.
Timu 12 zitashiriki mashindano hayo ambazo ni wenyeji Tanzania Bara, mabingwa watetezi Uganda, Kenya, Rwanda, Burundi, Somalia, Zanzibar, Sudan, Ethiopia na Malawi huku Zambia na Ivory Coast zikiwa ni waalikwa.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents