Promotion

Celtel yaja na mchingo mpya

Kampuni inayotoa huduma ya mawasiliano nchini ya Celtel, hivi karibuni imezindua huduma mpya iitwayo ‘one Office’ itakayowawezesha wateja wa mtandao huo kufanya shughuli za kiofisi katika nchi yoyote ya Afrika Mashariki na Kati bila kubadili simu zao.

Kampuni inayotoa huduma ya mawasiliano nchini ya Celtel, hivi karibuni imezindua huduma mpya iitwayo ‘one Office’ itakayowawezesha wateja wa mtandao huo kufanya shughuli za kiofisi katika nchi yoyote ya Afrika Mashariki na Kati bila kubadili simu zao.

 

Mkurugenzi mtendaji wa Celtel Tanzania bwana Bashir Arafeh alisema wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo mpya kuwa mteja wa mtandao huo hana haja ya kuingi gharama za usajili iwapo atahitaji kuwa mtumiaji wa huduma hiyo kinachotakiwa ni kuwa na simu yenye mtandao wa Celtel popote katika nchi yoyote ya Afrika Mashariki na Kati.

 

“Hakuna gharama za usajili na wala wateja hawahitaji kubadili miundo ya simu zao, wanachotakiwa ni kuhakikisha wanakuwa na simu zao wanapokuwa katika nchi za Afrika Mashariki na kati na kuendelea kutumia huduma hiyo kama vile wapo kwenye nchi zao” Bashir Arafeh alisema.

 

Wateja wa Celtel wataongeza muda wa salio katika simu zao kwa kutumia kadi za muda wa maongezi katika walizopo wakati wowote katika vituo vya mauzo vya Celtel zaidi ya 140,000 katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati, haitamlazimu mteja kuweka fedha nyingi kwenye simu au kununua vocha nyingi wakati wa kusafiri.

 

Mtandao huo ambao umejitosheleza kwa kiasi kikubwa saa utamuwezesha mteja kupata huduma ya intaneti, barua pepe na Celtal posta kama wanavyoweza kupata wakiwa kwenye nchi zao kwa kutumia huduma mpya na bora ya One Ofice.

 

“tukiwa kama kampuni bora ya mawasiliano nchini tuna jukumu la kuondoa vikwazo vya mawasiliano katika jumuiya ya Africa Mashariki na kati na sasa tunaonesha uaminifu na ubora wetu kwa kuboresha njia za mawasiliano kwa wateja wetu ili kuwafanya wawe karibu na ofisi zao na wapendwa wao popote pale safarini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents