Habari

CHADEMA waeleza kutoridishwa na kauli ya polisi kuhusu mikutano ya siasa

CHADEMA wameelezea wasiwasi wake juu ya tamko la jeshi la polisi kuhusu mikutano ya ndani na kusema kuwa hatua hiyo ni kuwapa mianya CCM.

salumpic

Kauli hiyo imetolewa na naibu katibu mkuu Chadema Zanzibar,Salum Mwalimu, baada ya jeshi polisi kuruhusu mikutano ya ndani kwa kuwa hali ya kisiasa nchini imetulia.

“Haiwezekani, na hii nadhani ni mara ya pili kwa jeshi la polisi,walifungia mikutano kipindi kile, halafu CCM walivyokuwa wakikaribia kwenye vikao vyao wakafungulia, halafu tena CCM walivyomaliza vikao vyao wakafunga,” amesema. “Kwahiyo kuna uwezekano mkubwa kwamba wanataka kuwapa nafasi chama cha mapinduzi, wafanye vikao vyao halafu utasikia amani imeteteleka tena kwahiyo tunavifungia tena vikao vya vyama vya siasa,” ameeleza Mwalimu.

“Kwahiyo wenye haki na mamlaka ya kufanya siasa wabakie chama cha mapinduzi kama ambavyo sasa hivi wanaendelea na mikutano yao,mwenyekiti wao anafanya mikutano, lakini mwnyekiti wetu hatakiwi kufanya mikutano,aliyekuwa mgombea wao anafanya mikutano,lakini aliyekuwa mgombea wetu wa urais haruhusiwi kufanya mikutano,hali hii ni ya hatari sana. Jeshi la polisi lijiangalie,lifanye kazi zake kwa weledi, lifanye kazi zake kwa utu na heshima, lifanye kazi zake kwa kusimamia sheria na haki, huo ndo wajibu wake,” aliomba.

Jeshi la polisi lilitoa tamko la kuruhusu mikutano ya ndani Septemba 22 mwezi huu chini ya kamishna wa jeshi la polisi CP Nsato Marijani.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents