Habari

CHADEMA wakaza uzi, wamtaka ajieleze kwanini wasimvue uanachama

Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA kimewaandikia barua za kuwavua rasmi nyadhifa za uongozi aliyekuwa naibu katibu mkuu Zitto Kabwe na wenzie sambamba na kupewa siku kumi na nne za kujieleza kwanini wasivuliwe uanachama kufuatia waraka wa siri waliouandika na kukamatwa hivi karibuni.

993397_615340251820009_638321306_n

Akizungumza na vyombo vya habari hapo jana mkurugenzi wa habari na uenezi wa CHADEMA, John Mnyika alisema barua hizo zilizoainisha makosa kumi na moja ya kukiuka katiba na itifaki za chama hicho, zitawataka wahusika kujieleza kwa maandishi na baadaye mbele ya chama kwa nini wasifukuzwe na kuvuliwa uwanachama kufuatia waraka waliouandaa uliosemekana ulilenga kikupindua chama hicho.

Mnyika aliongeza kuwa waraka huo uliochapisha kwenye baadhi ya magazeti na mitandao mbalimbali ya kijamii sio ule uliowahukumu wahusika hao na kuwaomba watanzania na wafuasi wa chama hicho kutoutilia maanani waraka huo na siku itakapobidi kuutoa waraka husika watafanya hivyo.

Akizungumzia mkutano uliofanywa na Zitto na wenzie licha ya kukata kusema hatua zitazozochukuliwa pindi watakaposhindwa kutimiza mashati waliyoyaweka, Mwanasheria mkuu wa chama hicho Tundu Lissu amesema mkutano huo ulilenga kupoteza lengo kuu la kuvuliwa madaraka na kuwa kilichowafukuza ni mkakati wao wa siri uliolenga kukipindua chama hicho na si vinginevyo.

Tundu Lissu aliongeza kuwa Zitto na wenzake hawajafukuzwa kwasababu ya taarifa za uongo za PAC,hawakufukuwa kwasababu ya posho,hawakufukuzwa kwasababu ya ya kuuza majimbo ya uchaguzi mwaka 2010,hawakufukuzwa kwaajili ya mambo mengine waliyoyataja bali wamefukuzwa kwa kuandaa mpango wa mapinduzi nje ya katiba ya chama, nje ya kanuni ya chama na nje ya namna ya kugombea uongozi nje ya chama.

Source:ITV

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents