Habari

CHADEMA wakubali kushiriki uchaguzi, Wasimamisha wagombea Kinondoni na Siha

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimekubali kushiriki uchaguzi mdogo wa majimbo mawili ya Siha na Kinondoni kwa kusimamisha Wagombea wawili kwenye nafasi ya ubunge.

Kupitia taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari, kupitia kwa Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema amesema kuwa kamati kuu ya chama hicho iliyokutana jana alhamisi jijini Dar es Salaam imefikia maamuzi hayo ya kushiriki kwenye uchaguzi mdogo kwenye majimbo ya Kinondoni na Siha unaotarajiwa kufanyika tarehe 19 Februari, 2018.

CHADEMA wamepitisha majina ya Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zanzibar, Salum Mwalimu kugombea Ubunge jimbo la Kinondoni na Bwana Elvis Christopher Mosi kugombea jimbo la Siha.

Awali chama hicho kilisusia kushiriki kwenye uchaguzi mdogo wa ubunge kwenye majimbo matatu ya Singida Kaskazini, Longido na Songea Mjini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents