Habari

CHADEMA wamvua uanachama Zitto Kabwe

Mwanasheria mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu ametangaza kuvuliwa rasmi uanachama kwa mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe.

Zitto akisisitiza jambo

Uamuzi huo umekuja baada ya chama hicho kushinda kesi dhidi ya Zitto. Mahakama imeamua katika hukumu yake leo kuwa chama kinaweza kuendelea na taratibu zake. Aidha, mahakama imeamuru Zitto alipe gharama zote za kesi.

Lissu amesema uamuzi huo umetokana na katiba ya CHADEMA, inayosema kuwa mwanachama anapofungua kesi dhidi ya chama, na kushindwa atakuwa amejiondoa uanachama wake.

“Kwahiyo natangaza rasmi rasmi Zitto Kabwe sio mwanachama tena wa Chadema na hii na kwa mujibu wa katiba ya chama,” amesema Lissu.

Hata hivyo Zitto ametumia Twitter kueleza kuwa hakuna na taarifa za kuitwa Mahakamani leo.

“Hatukuwa na wito wa mahakamani leo. Jaji kahamishiwa Tabora. Hatuna taarifa ya Jaji Mpya. Mwanasheria wetu anafuatilia na atatoa statement,” ameandika.

“Kwa sasa naendelea na kazi zangu kama kawaida. Leo nipo na EWURA kwenye PAC. Kesho TANESCO na Alhamis Mabilioni ya Uswizi. Kwa kazi ya #TegetaEscrow ilivyokuwa ingeshangaza waathirika kukaa bila kujaribu kunivuruga. Bahati mbaya sana sivurugiki. Ni Kazi tu.”

Novemba 22 mwaka jana, Zitto alisimamishwa unaibu Katibu Mkuu wa Chadema na unaibu kiongozi wa upinzani bungeni baada ya kutuhumiwa kuhusika na njama za kukihujumu chama hicho.

Zitto pia aliweka pingamizi mahakamani kuzuia kikao cha kamati Kuu kumjadili. Hoja yake ilikuwa ni kupinga kuitisha kamati kuu kabla shauri lake kusikilizwa na baraza Kuu.

Alidai anataka mahakama iagize kamati kuu ya CHADEMA kutojadili suala lake mpaka baraza kuu likae kuamua rufaa yake.

CHANZO: EATV (Twitter), Jamii Forums

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents