Habari

Chadema watoa neno kwa Wabunge wanaotimkia CCM

Katibu Mkuu wa  Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Vicent  Mashinji amesema wao hawana shida na suala la baadhi ya wanachama na  Wabunge wa chama hicho kutimkia CCM kwa sababu wanatumia haki yao ya kikatiba.

Dkt. Vicent Mashinji

Dkt. Mashinji amesema wabunge wanaohama na kujiuzulu  CHADEMA hawaiyumbishi  chama hicho tu bali wanayumbisha wadau wote wa uchaguzi pamoja na wananchi ambao ni walipa kodi, maana mchakato wa uchaguzi unatumia fedha na fedha hizo ni kodi za wananchi.

“Upande wa pili  umeamua  kujitoa ufahamu unafikiria kwamba kwa kufanya siasa za  kuwapa  watu rushwa wa upinzani kuhamia kwao kunadhohofisha  vyama vya upinzani, na kuwaahidi kuwapa nafasi zile zile walizokuwa nazo upinzani hata kama walishindwa kwenye kura za maoni”, amesema Mashinji.

Katibu huyo ameongeza kuwa tabia hiyo inaonekana wazi mpaka na ushahidi tayari ulishapelekwa kuanzia kwenye lile sakata la madiwani huko Arumeru walinunuliwa na Mh. Lema na Nassari walipeleka ushahidi TAKUKURU, hivyo CHADEMA haina shida nao wanaohama kwa sababu wanatumia haki yao kikatiba”, amesema Dkt. Mashinji.

Hivi karibuni upinzani umeondokewa na Mwenyekiti wa baraza la Vijana taifa (BAVICHA), Patrobas Katambi pamoja na Godwin Aloyce Mollel ambaye alikuwa Mbunge wa Siha (CHADEMA).

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents