Habari

Chadema yakanusha Mh. Mnyika kujivua uanachama

Baada ya taarifa kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Mbunge wa Kibamba , John Mnyika  kujivua Uanachama. Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), kimekanusha habari hizo na kusema kuwa habari hizo hazina ukweli wowote za zinapaswa kupuuzwa.

Chadema wametoa kanusho hilo kupitia mtandao wa Twitter, kupitia ukurasa wa chama hicho na kusema kusema kuwa wanaosambaza habari za Mnyika kujivua ni wale walioishiwa hoja na majibu juu ya maisha ya watanzania.

Kuna taarifa zinasambazwa mitandaoni ya kuwa Mhe. @jjmnyika, Mbunge wa Kibamba amejivua uanachama wa CHADEMA.
Taarifa hizo ni za uongo na hazina ukweli wowote, ni za kupuuzwa, wanaozisambaza ni wale walioishiwa hoja na majibu juu ya hali ya maisha ya Watanzania.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents