Michezo

Chama cha soka England (FA) chamfungia rasmi Schweinsteiger mechi 3

Chama cha soka cha England ( FA) kimetangaza rasmi kumfungia kiungo wa Manchester United, Bastian Schweinsteiger Mechi 3.

FA-Rungu-1

Adhabu hii inaanza mara moja baada ya Mjerumani huyo kuamua kutopinga mashitaka yake kwa kosa ambalo refa hakuliona na badala yake kuhukumiwa kwa ushahidi wa mkanda wa video.

wes

Schweinsteiger mwenye miaka 31, anadaiwa kumpiga beki wa West Ham Winston Reid kwa mkono walipokuwa wakigombea mpira wa free kick katika mechi ya ligi kuu England iliyomalizika 0-0 Jumamosi iliyopita.

Mwamuzi wa mechi hiyo, Mark Clattenburg, hakulitaja tukio hilo lakini aliongea na wachezaji wote wawili baada ya tukio lenyewe.

Katika taarifa yao, FA imesema kuwa tukio hilo lilipitiwa na waamuzi watatu tofauti ambapo kila mmoja aliafiki kuwa lilistahili kadi yyekundu na ndio maana wakafungua mashitaka dhidi ya Schweinsteiger.

Schweinsteiger atazikosa mechi za ligi dhidi ya Bournemouth, Norwich City na Stoke City na kurejea kwenye mechi na Chelsea.

Source: BBC

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents