Habari

Chama cha wafanyakazi Afrika Kusini (COSATU) chamkalia kooni Zuma

Chama kikuu cha wafanyakazi nchini Afrika Kusini, Cosatu kimeunga mkono juhudi zinazoendelea za kumtaka Rais Jacob Zuma kujiuzulu.

Chama hiko cha wafanyakazi kinakiunga mkono chama tawala cha nchi hiyo lakini wanamtaka Zuma kujiuzulu kwa kile wanachokitaja kuwa na uhusiano wa karibu na familia moja ya jamii ya wahindi nchini humo ijulikanayo kama Gupta.

Inadaiwa kuwa familia hiyo ina nguvu kubwa ya ushawishi mkubwa katika serikali ya Rais Zuma. Hali ya uchumi wa Afrika Kusini imekuwa ikiyumba tangu aliyekuwa waziri wa fedha nchini humo Pravin Gordhan kufutwa kazi wiki iliyopita.

Kwa sasa macho yote yanaelekezwa katika kamati ya kazi ya chama cha ANC ambacho kinafanya mkutano kuhusu kiongozi huyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents