Habari

Chama cha wafugaji chalaani tukio la kuchomwa mkuki mkulima

Chama cha wafugaji nchini, kimelaani vikali kitendo cha mfugaji kujichukulia hatua na kumchoma mkulima mmoja aliyejulikana kwa jina la Augustino Mtitu aliyechomwa mkuki mdomoni na hatimaye mkuki huo kutokea shingoni.

Akizungumza kwenye ofisi za chama cha waandishi wa habari mjini Morogoro, Naibu katibu mkuu wa chama cha wafugaji Tanzania, Joshua Lugaso pamoja kulaani kitendo hicho amewataka waandishi wa habari kuripoti sawa matukio yote yanayohusu wakulima na wafugaji.

Lugaso ameyaasa makundi ya wakulima na wafugaji kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi pindi zinapoibuka tofauti baina yao, badala yake watumie meza kwa mazungumzo na kuviachia vyombo vya dola kuchukuwa mkondo wake, kwa vile hakuna chochote kinachofanana na thamani ya maisha ya binadamu.

Tukio hilo limetokea Disemba 25, mwaka huu katika kijiji cha Dodoma Isanga kata ya Masanze wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents