Habari

Chama cha Wanahabari Wanawake nchini chaitaka NEC kuweka sheria kali Uchaguzi Mkuu

Chama cha Wanahabari Wanawake nchini (TAMWA) kimeiomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuweka sheria kali kwa makundi na viongozi ambao wanatumia nafasi zao kuwadhalilisha na kubana nafasi ya wanawake kushiriki katika uchaguzi mkuu.

Mkurugenzi wa Tamwa Rose Ruben akizungumza na vyombo vya habari

Hadi kufikia leo tamko hili likitolewa na Mkurugenzi wa Tamwa Rose Rubean takwimu zinaonyesha ni wanawake wawili tu ambao wamejitokeza kugombea nafasi ya juu ya urais pia wanawake watano wakitambulishwa kuwania nafasi ya umakamu wa urais, hii ikionyesha ushiriki mdogo sana wa wanawake kujitokeza hali inayopelekea kuziweka bayana changamoto zinawakabili wanawake.

Aidha, imeelezwa kuwa lugha za kudhalilisha kwa wanawake hasa katika kipindi cha uchaguzi huwadhoofisha sana wanawake huku wakizitaka mamlaka husika kudhibiti vitendo vya rushwa ya pesa na ngono kwa kuwa huleta adha kubwa kwa jamii.

Rose ameziomba pia jumuiya mbalimbali za wanawake kwenye vyama vya siasa kuhakikisha uwazi unakuwepo pamoja na uthubutu wa wanawake kuzidi kujitokeza zaidi katika kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 28.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents