Fahamu

Chama cha ‘wanaume wachoyo’ chaanzishwa Nigeria (+ Video)

Taarifa kuhusu chama cha wanaume wachoyo cha Nigeria- Stingy Men Association of Nigeria (Smen), imeenea kwenye mtandao wa kijamii waTwitter nchini Nigeria huku wanaume maarufu wa Nigeria wakishirikisha umma kadi za uanachama wao wa kikundi hicho.

Ujumbe wa Twitter wa mzalishaji wa muziki Don Jazzy wa kadi yake ya uanachama ulishirikishwa tena na wafuasi wake mara 11,000.

Nyota wa muziki wa Afrobeats Bw Eazi pia alituma kati yake ya uanachama katika chama cha wanaoume wachoyokupitia mtandao wa Twitter:

Akaunti rasmi ya chama cha wanaume wachoyo kwenye mtandao wa Twitter ilionekana kwenye mtandao huo kwa mara ya kwanza Jumatatu:

Wanaotuma jumbe za Tweeter wamekuwa wakitania kuwa watabuni wimbo wao maalumu, makao makuu na kiapo.

Haijawa wazi ni vipi taarifa ya chama cha wanaume wachoyo iliyoshirikishwa zaidi kwenye Twitter ilivyoanza nchini Nigeria. Wazo hilo tayari limesambaa katika mataifa mengine ya Afrika.

Mwezi Disemba taarifa ya gazeti la Uganda la Daily Monitor iliainisha pendekezo la kikundi hicho nchini Uganda.

Katika taarifa hiyo iliyoandikwa na , Ian Ortega aliandika: “Katiba hii iliandikwa katika mwaka wa janga la corona itaelezea maana ya hatua hatua kali .”

Sehemu ya”katiba yake ” iliwalengamarafiki wa kike wanaowaomba wapenzi wako wa kiume pesa.

“Kila binti wa Eva ambaye anaomba pesa atachukuliwa kama muhamiaji haramu na kuepukwa; ‘hafai kuwa mke ,’” aliandika.

Aliendelea kusema kuwa “mjumbe hapaswi kuhisi aibu yoyote katika kukataa ombi lolote la pesa linalowasilishwa kwake.”

Hii ni pamoja na maombi ya pesa za usafiri au salio la simu.

Bofya hapa chini;

https://www.instagram.com/tv/CJ-ssbEBANK/

https://www.instagram.com/tv/CJ-ssbEBANK/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents