Habari

‘Chambua Kama Karanga’ ya Saida Karoli yatumika kwenye filamu mpya ya Tyler Perry ‘Peeples’

Msanii wa muziki wa asili nchini Saida Karoli amesema amefurahishwa na kitendo cha mtayarishaji na muigizaji maarufu wa filamu nchini Marekani, Tyler Perry aliyeutumia wimbo wake ‘Maria Salome aka ‘Chambua Kama Karanga’ kwenye filamu ya mpya, Peeples.

Akiongea na kipindi cha Take One cha Clouds TV, Saida alisema yeye mwenyewe alikuwa hatambui kama wimbo wake umetumika kwenye filamu hiyo ya Kimarekani na baada ya kupata taarifa hizo alisema alifurahshwa kwakuwa hiyo ni njia ya kuitangaza asili ya Mtanzania.

“Nitakuwa nimejisikia vyema kwasababu ukiona nyimbo zinakubalika kiasi hicho na hisi nchi yetu ya Tanzania itakubalika zaidi na zaidi kwamba asili ya Mtanzania ni nini,” alisema Saida.

Kwenye filamu hiyo, mmoja wa waigizaji wa filamu hiyo anaonekana akijifunza kucheza wimbo huo.

Peeples ni filamu ya Kimarekani ya mwaka huu iliyoandikwa na Tina Gordon Chism na kutayarishwa na Tyler Perry. Waigizaji kwenye filamu hiyo ni pamoja na Craig Robinson na Kerry Washington na May 10, 2013.

Albam yake ya kwanza, ‘Maria Salome’ ilizinduliwa tarehe 2 Septemba mwaka 2001 na ilipachikwa jina la Chambua kama Karanga na mashabiki kutokana na maneno aliyokuwa akiimba kwenye wimbo Maria Salome.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents